


In case of crashes or set the name, as well auto backup function with misale ya waumini pdf possibility to remove old archives. Itakumbukwa kwamba, tafsiri hii ni ile inayotolewa kutoka katika Lugha ya Kilatini. Hii ni kazi iliyofanywa na Kikosi kazi cha Watu 10 kutoka Kenya na Tanzania na kufanya tathmini yao ya pamoja hivi karibuni, Kurasini, Jijini Dar Es Salaam. Askofu Salutaris Libena, Mwenyekiti wa Idara ya Liturujia, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Ifakara, anabainisha kwamba, Misale ya Altare kwa lugha ya Kiswahili inatarajiwa kutolewa kabla ya mwisho wa Mwaka 2015. Kwa kutambua umuhimu wa mabadiliko yaliyofanywa kwenye vitabu vya Liturujia hivi karibuni, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA wakati wa maadhimisho ya mkutano wake wa 18 uliofanyika nchini Malawi, kwa pamoja waliamua kwamba, Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Kenya na Tanzania kushirikiana kwa pamoja ili kuandaa Misale ya Altare kwa lugha ya Kiswahili, itakayotumiwa na wazungumzaji wa Kiswahili ndani na nje ya Nchi za AMECEA. Hii inatokana na ukweli kwamba, Kanisa ni Sakramenti ya Umoja.
